MISHAHARA ILIPWE KUANZIA APRIL 14.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dk.Hussein Ali Mwinyi ameagiza malipo ya mishahara ya mwezi wa April kufanyika mapema kuanzia tarehe 14 April 2023 kwa wafanyakazi wa Serikali kwa ajili ya matayarisho ya Sikukuu ya Eid El Fitr.

Kwa mujibu wa tamko la Rais Dk. Mwinyi hatua hiyo imelenga kuwapa wafanyakazi Serikalini muda wa kutosha wa kufanya maandalizi ya sherehe za Eid El Fitr.

Sherehe hizo zinatarajiwa kuangukia kati ya siku ya Ijumaa au Jumamosi ya tarehe: 21 au 22 April 2023 kutokana na kuandama kwa mwezi na kuashiria mwisho wa Ramadhan.

Aidha, Rais Dk. Mwinyi alitumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyakazi wa Serikali kwa ushirikiano wao wakati wa ibada tangu kuandama kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)