WATALAAM WASHIRIKI KIKAO KAZI CHA UTOAJI HUDUMA YA AFYA YA AKILI

0

 





Wataalamu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wameshiriki Kikaokazi cha utoaji wa huduma ya afya ya akili, msaada wa kisaikolojia na kijamii, kinachofayika Jijini Dodoma Maçhi 24 - 25,2023.



Kikaokazi hicho, Kimejadili namna ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa makundi yaliyo katika mazingira hatarishi na jamii kwa ujumla.

Akifuzungumza wakati wa kikao hicho, Kamishna  Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Baraka Makona amewasa wadau kuhakikisha huduma ya afya ya akili, msaada wa kisaikolojia na kijamii zinafika kwenye jamii.


Wizara zingine za kisekta zilizo shiriki ni pamoja na, Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Uratibu na Bunge, ORTAMISEMI, UTUMISHI, Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na Wizara ya Afya.


Wadau wengine ni pamoja na Mwenyekiti wa Maafisa Ustawi wa Mikoa, Mwenyekiti wa Waratibu wa Afya Akili Mkoa, WHO, UNICEF, PACT, HelpAge, na Conscious Mind.

MWISHO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)