WAKAZI WA MAJANI YA CHAI JIJINI TANGA WAPONGEZWA KUKIPAMBANIA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KUPATA KIWANJA CHA KUJENGA KAMPASI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amewapongeza wakazi wa Majani ya Chai Kata ya Maweni jijini Tanga kwa kukipambania Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kupata eneo la kujenga kampasi itakayokuwa na manufaa ya vizazi vyao, kwa wakazi wa mkoa huo na Watanzania wote watakaopata fursa ya kupata elimu katika kampasi hiyo pindi ujenzi wake utakapokamilika.

Mhe. Jenista ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na wananchi wa Majani ya Chai Kata ya Maweni jijini Tanga alipoenda kuwatembelea kwa lengo la kuwashukuru kwa kukiunga mkono Chuo cha Utumishi wa Umma kupata umiliki wa kiwanja ili kujenga kampasi jijini humo.

Mhe. Jenista amesema kuwa, wakazi wa Majani ya Chai jijini Tanga wametoa somo kwa Watanzania kwani maeneo mengine, Serikali ikitaka kujenga miundombinu endelevu kwenye eneo lenye mgogoro wa ardhi mara nyingi wananchi wanakuwa upande wa wanaodai kumiliki viwanja licha ya kushindwa kuviendeleza, hivyo wananchi wa Majani ya Chai wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kupambania ujenzi wa chuo kwa manufaa ya taifa. 

“Nimefurahishwa sana na uamuzi wenu wa kulilinda na kulipambania eneo hili na hatimaye Chuo cha Utumishi wa Umma kimepata kiwanja cha kujenga kampasi na kuongeza kuwa, limekuwa ni somo tosha ya namna ya kuisaidia Serikali kupata eneo la kujenga miundombinu yenye tija kwa Serikali na wananchi pia,” Mhe. Jenista amesisitiza.

Mhe. Jenista amesema, changamoto iliyokuwepo ilikuwa ni upatikanaji wa eneo la kujenga kampasi ya chuo jijini Tanga, hivyo amemshukuru Kamishna wa Ardhi jijini Tanga kwa kutoa taarifa rasmi kuwa kiwanja hicho ni mali ya Chuo cha Utumishi wa Umma mara baada ya kufanyika kwa mchakato wote wa kisheria wa umilikishaji ardhi kwenye eneo lililokuwa na mgogoro. 

“Tumejipanga kujenga kampasi yetu wenyewe kwani tunapanga jengo la kuendesha shughuli za chuo ambalo linatugharimu shilingi milioni 84 kwa mwaka, hivyo leo wananchi wa Majani ya Chai mmeokoa fedha hiyo ya Serikali

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)