Na Elimu ya Afya kwa Umma Kagera.
ganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ametoa taarifa ya muendelezo kuhusu mlipuko ugonjwa wa Marburg uliyoibuka Katika Mkoa wa Kagera na hatua mbalimbali zinazoendelea chukuliwa na Serikali katika Kudhibiti ugonjwa huo.
Prof. Nagu ametoa taarifa hiyo mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera kwa ajili ya kuangalia jitihada zinazofanyika katika kupambana na ugonjwa huo, Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Nagu amesema kuwa hadi kufikia Jana hali ya kuenea kwa ugonjwa imeendelea kudhibitiwa kwani hadi Jana saa 6 usiku Jumla ya wagonjwa walioambukizwa ni 8, Huku idadi ya Waliofariki ni 5 na wagonjwa watatu wakiendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri ambapo amesema '' *Hali ya ugonjwa kudhibitiwa inaendelea vizuri kwani pamoja na hao walioambukizwa lakini tunaendelea kuwafatilia wale walio tengamana na wagonjwa ambao tayari walikuwa na maambukizi ambao Jumla yao ni 193 na kati ya hao Wataalamu wa Afya ni 89 na Wananchi wa kawaida ni 104 na tutaendelea kuwafatilia kwa siku 21 kujua maendeleo yao''*
Aidha Prof. Nagu ameongeza kuwa Jitihada mbalimbali zimeendelea kuchuliwa ili Kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kuendelea kutoa elimu ya Afya kwa Wananchi Jinsi ya kujikinga na kutoa vipeperushi vyenye ujumbe wa kuelimisha nakutumia magari maalumu ya kutolea matangazo mitaani, Magonjwa haya ya Mlipuko mara nyingi huwa hayana Tiba maalumu badala yake katika Kudhibiti huwa tunaishirisha Jamii katika kuwapa Elimu lakini kama mnavyojua kuwa ugonjwa huu hauna Tiba ila Huwa una dalali za aina tofauti na mtu anapogundulika kuwa na dalili huwa anaanza kutibiwa dalili hizo ambazo ni homa ,mwili kuishiwa nguvu ,kichwa kuuma ,kutokwa na damu katika maeneo ya wazi,videonda vya koo , maumivu ya misuli .
Katika hatua nyingine Prof. Nagu ameongeza kuwa tayari Wizara ya Afya imeongeza Timu ya Wataalamu ambao ni Madaktari Bingwa na Bobezi 15 wakiwemo wa Figo kuja kuongeza nguvu katika Mkoa wa Kagera katika kukabiliana na ugonjwa wa Marbug
Pia Serikari kupitia Wizara ya Afya imeongeza ufuatiliaji na udhibiti wa ugonjwa wa huo kuanzisha Upimaji wa Afya katika maeneo ya Bandarini ,Mipakani na kwenye vituo vya mabasi.
Katika hatua nyingine Prof. Nagu ametoa pole kwa Mkoa wa Kagera pamoja na familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na ugonjwa wa Marburg.
Wizara ya Afya tayari imeshatuma Timu mbalimbali za Wataalamu kwa ajili ya kufatilia wahisiwa na kutoa Elimu kwa Wananchi kuweza kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Marburg ambapo Njia zinazo shauriwa na wataalamu katika kujikinga na ugonjwa huo ni Kunawa Mikono kwa Sabuni na maji tiririka ,kutumia vipukusi (sanitizer) kuto kusalimiana kwa kupeana Mikono ,kutokuwa karibu na wanyama mbalimbali kama vile Popo,Ngedere,Swala na wanyama wengine wa Porini pia kuto tumia Mavazi ,matandiko ,kinyesi,matapishi,jasho na damu na endepo utamuona mtu mwenye dalili hizo basi piga simu namba 199 au kutoa taarifa katika Ofisi ya serika ya mtaa, Kijiji au katika Vituo vya kutolea huduma za Afya .