KIKUNDI CHA WALEMAVU CHA USHONAJI VIATU KIMEMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUNUFAIKA NA MIKOPO YA HALMASHAURI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Kikundi cha Watu wenye ulemavu kinachojihusisha na ushonaji viatu cha Pcohekago katika Manispaa ya Mpanda kimemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwawezesha Walemavu kunufaika na Mikopo inayotolewa na Halmashauri ambapo mpaka sasa kimekopeshwa shilingi milioni 19 katika nyakati tofauti.

Salamu za Shukurani zimetolewa na Kikundi hicho wakati kilipotembelewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ikiongozwa na Mhe. Stanslaus Mabula (Mb) kwa aijli ya kukagua maendeleo ya Kikundi hicho.

Wakati akisoma taarifa Mwenyekiti wa kikundi hicho, Bw. Plasido kameme amesema awali kikundi kilikopa mkopo wa shilingi milioni 8 mwaka 2019/2020 na kuzitumia kushona viatu na kubrashi, kushona kuuza nguo, kununua na kuuza mazao ambapo Kikundi kilifanikiwa kurejesha fedha kwa wakati.

Aidha, Mwenyekiti wa Kikundi, Bw. kameme ameeleza mwaka wa fedha wa 2020/2021 kikundi kilipokea Mkopo awamu ya pili kiasi cha shilingi milioni 11 ambapo zinaendelea kutumika kuendeleza biashara walizonazo.

Bw. Plasido kameme amesema faida waliyoipata kutoka na Mikopo imewawezesha kujenga nyumba za kuishi kila mwanakikundi na kuboresha miradi ambayo wanaendelea kuiendesha.

Kwa Upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mhe. Stanslaus Mabula amepongeza kikundi kwa kutumia fursa ya kujiunga kwenye vikundi kwa kupata mikopo ambayo haina riba. 

Mabula amesema Kamati ya LAAC inaendelea kufuatilia wanufaika wa Mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ili kujiridhisha kama Mikopo inayotolewa na Halmashauri inawafikia walengwa na kuleta tija.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)