WANANCHI WATAKIWA KUACHA KUKOPA FEDHA BILA MALENGO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Gideon Gregory, Dodoma.

Wananchi nchini wametakiwa kuacha kukopa fedha bila malengo badala yake watumie mikopo kama fursa ambazo zitawasaidia kupiga Hatua kimaendeleo.

Hayo yamebainishwa leo Februari 14,2023 na Katibu mtendaji Mkuu wa Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi Beng'i Issa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema kupitia Baraza la Uwezeshaji wananch kiuchumi wameunda njia Mbalimbali ambazo zitawasaidia wananchi kunufaika na Baraza Hilo la kuwezesha wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko ya mikopo ya jamii ambayo kwasasa kuna jumla ya mifuko 72 ili kuwanufaisha wanchi wote walio Katika mifuko hiyo ya jamii.  

Amesema baraza hilo linafanya kazi kwa kufuata na kusimamia sera ya Taifa ya Uwezeshaji yenye nguzo mbalimbali na NEEC ndio chombo pekee kinachosimamia ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati (Local Content) nchini.

“Baraza hili linashughulikia miundombinu ikiwemo barabara, biashara, umeme kwani vitu hivi kama umeme kwasasa ni muhimu sana kwa Dunia ya sasa kwasababu kwasasa watu wengi wanatumia umeme kwaajili ya kuendesha shughuli zao kama biashara hivyo sisi kama secta ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi tunaendelea kusimamia secta hizo ili Kila mmoja anufaike na Baraza letu,”amesema.

NEEC inasimamia programu za uwezeshaji (Viwanda Scheme) ambazo ni wafanyabiashara wenye viwanda vidogo na vya kati hukopeshwa na mpaka sasa imewezesha kuwapatia zaidi ya Shilingi Bilioni 3.5 wafanyabiashara wenye viwanda vya kati na vidogo katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini.

“Watanzania zaidi ya 83,000 wamepata ajira ya kimkakati na hadi sasa imewezesha kuwapatia Bilioni 3.5 wenye viwanda vya Kati na vidogo Katika miradi 62 kwenye mikoa 12 nchini na pia baraza huandaa makongamano kwaajili ya maonesho kwa lengo la kuendelea kutoa elimu kwa wananchi,”amesema.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)