BRICS YAIPIKU G-7 KATIKA UKUAJI WA UCHUMI DUNIANI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Ripoti mpya ya Benki ya Dunia inaeleza kuwa nchi wanachama wa kundi la BRICS zimezitumulia kivumbi nchi za kundi la G-7 katika kiwango cha ushiriki kwenye ukuaji uchumi duniani.

Benki ya Dunia imetangaza katika ripoti yake mpya kuwa, kiwango cha ukuaji wa uchumi wa nchi wanachama wa kundi la BRICS ambazo ni Russia, China, India, Brazil na Afrika Kusini mwaka 2023 kimefikia asilimia 32.1. Ripoti hiyo imesema ukuaji huo wa kiuchumi umepita ule wa nchi wanachama wa kundi la G-7 linaloundwa na Ujerumani, Ufaransa, Italia, Japan, Uingereza, Canada na Marekani. 

Ripoti mpya ya Benki ya Dunia imeongeza kuwa, kiwango cha ushiriki wa nchi wanachama wa kundi la BRICS katika ukuaji uchumi duniani mwaka 2028 kitafikia aslimia 33.3 kwa mujibu wa makadirio yaliyofanywa. 

Ripoti hiyo imeendelea kueleza kuwa, mchango wa nchi wanachama wa G-7 katika ukuaji uchumi duniani mwaka huu wa 2023 umefikia asilimia 29.9; kiwango ambacho kitafikia asilimia 27.8 ifikapo mwaka 2028. Kiwango hicho kinatajwa kuwa cha chini zaidi ikilinganishwa na takwimu za nchi wanachama wa kundi la BRICS. 

Chanzo #Parstoday.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)