PANYAA WAVAMIA ZAIDI YA HEKA 1000 KAHAMA

0


Wakulima katika kata ya Mwalugulu halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wameingiwa na hofu ya kukumbwa na njaa kutokana na zaidi ya Heka Elfu Moja [1000] za mazao ya mahindi na mpunga Kuvamiwa na kundi kubwa la panya.
Wakizungumza na kipindi hiki baadhi ya wakulima hao Malale Mihambo, Kabula Bukwimba,Lushishi Peter na Embasi Mbucha wote wakazi wa kata ya Mwalugulu halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga ,wamesema kuwa kundi kubwa la panya kushambulia mazao yao pindi wanapopanda imekuwa ni changamoto kubwa hali hiyo ni dalili ya kukumbwa na janga la njaa.
Ngusa Mayunga ni mwenyekiti wa kijiji cha sungamile kilichopo kata ya Mwalugulu ambapo amebainisha kuwa katika kijiji chake zaidi ya heka mia mbili [200]za mazao ya mpunga na mahindi zimeshambuliwa na panya kwa kipindi cha mwezi Novemba hadi Disemba mwaka huu ambapo panya wamekuwa wakifukua mbegu pindi zipandwapo mashambani huku akiimba serikali kulifanyia ufumbuzi tatizo hilo.
Kwa upande wake Afisa kilimo wa kata ya Mwalugulu halmashauri ya Msalala ,Mwaki Jale amesema kuwa taarifa za shambulio la panya katika kata yake ameshazipokea na kuzipeleka katika ngazi ya halmashauri huku akibainisha kuwa katika kata yake ni zaidi ya heka elfu moja za mazao ya mpunga na mahindi zimeshambuliwa na panya.
Kata ya Mwalugulu ni miongoni mwa kata zinazounda halmashauri ya Msalala ambayo imeundwa na vijiji vya Sungamile,Mwalugulu,Banhi,Kilimbu na Mwankima ambavyo katika msimu huu wa kilimo vimekumbwa na wimbi kubwa la panya kushambulia mazao ya mpunga na mahindi mashambani.
Na.Faustine Gimu Galafoni.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)